Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kushirikiana na Benki ya Biashara ya Taifa (TCB) limezindua kadi maalumu ya kidigitali kwa ajili ya kununua tiketi za treni, ikiwa ni hatua ya kuimarisha huduma na kukuza uchumi wa kidigitali nchini.

Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TRC, Frederick Massawe, amesema mfumo huo utaongeza ufanisi wa usafiri wa reli, kupunguza matumizi ya fedha taslimu na kuboresha usimamizi wa mapato.

Aidha, amesema utarahisisha huduma kwa abiria, kuvutia uwekezaji zaidi katika miundombinu na kuchochea mzunguko wa fedha kupitia mifumo ya kibenki.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *