#HABARI: Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Utoaji Bora wa Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2025 kwa taasisi za Serikali zinazotoa huduma ya nishati katika tukio la tuzo hizo zilizofanyika katika wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza tarehe 6 – 10 Oktoba 2025.

Tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kuzikutanisha taasisi na kampuni mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi zenye zinazotoa huduma mbalimbali nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah ambae pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi alizipongeza taasisi zote zilizoshiriki na kuonyesha ubunifu katika utoaji huduma, huku akisisitiza kuwa taasisi za umma zina wajibu mkubwa wa kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wananchi kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya wateja.

“Niwapongeze wenzetu ambao wamepata hizi tuzo na wale walioandaa kwa sababu tunapowapa hizi tuzo inawasaidia kuwaonyesha kile wanachokifanya kinafuatiliwa kwa karibu. Taasisi zote ambazo zimepata tunazifahamu na tunaeelewa umuhimu mkubwa kwa kila wanachokifanya. Kwa wale ambao hawajapata nao wameona ipo namna ya kwenda kuboresha huduma zao,” alisema Dkt. Abdallah.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *