Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), limezindua rasmi Programu Tumizi “App” ya Utalii inayolenga kupanua wigo wa utoaji taarifa za vivutio vya utalii ikiwemo hifadhi zote za Taifa na taratibu za ulipaji wa vibali vya kuingia katika hifadhi kwa watalii bila kupitia kwa mawakala.
Akizindua programu hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas amepongeza juhudi za TANAPA za kutangaza utalii kupitia teknolojia hususani programu tumizi inayopatikana katika simu janja za viganjani na kuongeza kuwa itaongeza wepesi wa watalii kutembelea vivutio hivyo.
Mhariri @moseskwindi