#HABARI: Jumuiya ya wasioona Tanzania imewataka vijana kutokubali kutumika na watu wa nje kuleta mafarakano ndani ya nchi yao ili kuepusha maafa yanayoweza kuikumba jamii likiwemo kundi la watu wenye ulemavu

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo….wakati wa hafala ya chakula cha pamoja kilichoandaliwa na wahisani kwa ajili ya kundi hilo ambapo pamoja na mambo mengine ameelezwa kuguswa na hatua ya Rais Samia kwa kutengeneza ilani iliyogusa makundi yote kwenye jamii wakiwemo kundi la watu wasioona.

Naye Mjumbe wa kamati kuu wa Chama cha Mapinduzi Ruchard Kasesela amesema Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake ameonesha moyo wa pekee kwa kundi hilo hivyo kuiasa jamii kuwa kitu kimoja katika kuliwezesha kundi hilo ili liweze kujikwamua kiuchumi.

Aidha katika kutambua mchango wa Dkt.Reginald Mengi la kuwasadia watu wenye mahitaji maalumu kwenye jamii Kasesela ameahidi kushirikia na wadau wengine kihakikisha kazi hiyo inaendelezwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *