London, England. Meneja wa England, Thomas Tuchel jana ametangaza kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mechi mbili za kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 wiki ijayo dhidi ya Serbia na Hungary wiki ijayo huku akiwarudisha kikosini baadhi ya mastaa na wengine akiwatema.

Katika kikosi hicho, Tuchel amewajumuisha Phil Foden wa Manchester City na Jude Bellingham wa Real Madrid ambao hakuwaita awamu iliyopita.

Hata hivyo Tuchel hawajaita kikosini, Trent Alexander-Arnord wa Real Madrid na Myles Lewis Skelly wa Arsenal.

Meneja huyo amemuita kwa mara ya kwanza kiungo wa Bournemouth, Alex Scott lakini hajawapa nafasi Jack Grealish wa Everton na mshambuliaji Danny Welbeck wa Brighton.

Makipa wanaounda kikosi cha England ni Dean Henderson (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton) na Nick Pope (Newcastle Utd.

Mabaki ni Dan Burn (Newcastle United), Marc Guehi (Crystal Palace), Reece James (Chelsea), Ezri Konsa (Aston Villa), Nico O’Reilly (Manchester City), Jarell Quansah (Bayer Leverkusen), Djed Spence (Tottenham Hotspur) na John Stones (Manchester City).

Timu hiyo ina viungo Elliot Anderson (Nottingham Forest), Jude Bellingham (Real Madrid), Jordan Henderson (Brentford), Declan Rice (Arsenal), Morgan Rogers (Aston Villa), Alex Scott (Bournemouth) na Adam Wharton (Crystal Palace).

Kwa upande wa washambuliaji kuna Jarrod Bowen (West Ham United), Eberechi Eze (Arsenal), Phil Foden (Manchester City), Anthony Gordon (Newcastle United), Harry Kane (Bayern Munich), Marcus Rashford (Barcelona, loan from Manchester United), na Bukayo Saka (Arsenal).

England inashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Kundi K la kuwania kufuzu Kombe la Dunia ikiwa na pointi 18.

Novemba 13, 2025, England itakuwa nyumbani kukabiliana na Serbia na siku tatu baadaye itaifuata Albania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *