Wiki iliyopita Waendesha mashitaka Tanzania waliwafungulia kesi ya Uhaini takriban watu 240, kufuatia maandamano ya vurugu yaliyotokea wakati wa uchaguzi huku taifa hilo likipitia hali ya mashaka ya kisiasa kutokana pia na vifo vya watu wengi vinavyodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama wakati wakijaribu kudhibiti ghasia hizo za baada ya uchaguzi.