Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limekamata meli ya mafuta katika pwani ya kusini ya Makran baada ya kupokea amri ya mahakama.

Ofisi ya mahusiano ya umma ya Kikosi cha Wanamaji cha IRGC imetangaza Jumamosi kwamba vikosi vyake vya uchukuaji hatua za haraka vilianza kuifuatilia kwa karibu meli ya mafuta ya Talara yenye bendera ya Visiwa vya Marshall mnamo saa moja na nusu asubuhi siku ya Ijumaa baada ya mahakama kutoa amri ya kuzuiliwa shehena ya mizigo ya meli hiyo.

Taarifa ya ofisi hiyo imesema, meli hiyo ya mafuta, ikiwa imebeba tani 30,000 za vifaa na mada za petrokemikali na ikiwa njiani kuelekea Singapore, iliongozwa kutia nanga kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana na ukiukaji iliofanya.

Kikosi cha Wanamaji cha IRGC kimebainisha katika taarifa hiyo kwamba “operesheni hiyo ilifanyika kulingana na majukumu ya kisheria na kwa ajili ya kulinda maslahi ya taifa na rasilimali za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.”

Taarifa ya kikosi hicho cha Wanamaji cha IRGC imebainisha kuwa meli hiyo, shehena yake, na nyaraka zake zilichunguzwa kikamilifu, na kwamba meli hiyo imepatikana na hatia ya “kubeba shehena isiyo na kibali.”

Maafisa wa Marekani walitangaza jana Ijumaa kwamba Talara ilikuwa ikisafiri kutoka Ajman, Muungano wa Falme za Kiarabu, kuelekea Singapore wakati vikosi vya IRGC vilipoizuia.

Kituo cha Operesheni za Biashara za Baharini cha jeshi la Uingereza ncho pia kiliripoti kukamatwa kwa meli hiyo ya mafuta, na kukiri kwamba Talara ilikuwa imeelekezwa kwenye maji ya eneo la Iran.

Itakumbukwa kuwa, mnamo Mei 2022, vikosi vya IRGC vilikamata meli mbili za mafuta za Ugiriki na kuzishikilia hadi Novemba mwaka huo kwa ukiukaji wa sheria.

Aidha, mnamo mwezi Aprili 2024 viliichukua meli ya mizigo ya MSC Aries yenye bendera ya Ureno katika Mlango-Bahari wa Hormuz…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *