Watu watatu akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 65, wamekamatwa na askari wa maliasili kwa madai ya kukutwa wakilima ekari tisa za dawa za kulevya aina ya bangi katika Kijiji cha Kapanga – Tanganyika, mkoani Katavi.

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Onesmo Buswelu ametoa onyo kwa wananchi wanaoendelea kulima bangi katika hifadhi za misitu iliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji wa mradi wa hewa ya ukaa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *