#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani imewahukumu Mohamed Juma Mohamed (Mudy Mweusi), miaka 23, Dereva bodaboda, Mkazi wa Mtongani – Mlandizi na Ashrafu Adam Kida (Shila), miaka 19, Fundi Makenika, Mkazi wa Kidile- Mlandizi kifungo cha maisha jela na kulipa fidia kiasi cha shilingi milioni 10 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka kwa pamoja binti wa miaka 18.

Hukumu hiyo ya kesi namba 10468/2025 imesomwa Desemba 01, 2025 na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mhe. Fredrick Shayo baada ya upande wa Mashtaka kuthibitisha kosa hilo bila kuwepo na shaka lolote.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Februari 03, 2025 huko maeneo ya barabara ya Halmashauri ya Mlandizi, Wilaya ya Kibaha ambapo binti huyo alikodi pikipiki kutoka Mlandizi kuelekea Ruvu Stesheni ndipo akiwa njiani dereva alisimamisha pikipiki kisha wenzake wawili ambao aliounga nao njama walifika eneo hilo na kuanza kumbaka binti huyo.

Mheshimiwa Shayo alieleza kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1), 131 (1) na 131 A (1) na (2) vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *