HABARI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeibuka Mshindi wa kwanza wa jumla katika tuzo ya Uandaaji wa Hesabu za Kifedha zinazozingatia viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (IPSAS), zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Pia imeibuka mshindi wa kwanza katika tuzo ya kipengele cha Taasisi za Serikali (Government Agency Categories). Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha Laurent Luswetula, amezipongeza taasisi zilizoibuka na ushindi, huku akisema wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa NBAA, ili kuendelea kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora.

Pia alisema Serikali itahakikisha NBAA inasimama imara ili iendelee kuzalisha watendaji bora kwa maslahi mapana ya taifa.”Wizara ya fedha itaendelea kuhakikisha inatoa ushirikiano kwa NBAA ili kuzalisha wahasibu na wakaguzi bora kwa mslahi mapana ya taifa letu,” alisema.

Huku kwa upande wake Naibu Kamishina Mkuu wa TRA Mcha Hassan Mcha alisema, tuzo waliyopata ina umuhimu mkubwa, kwani inachangia kuonesha utendaji wao unakubalika Kimataifa. Pia alisema tuzo hiyo inaonesha umahiri na ubunifu uliyopo kwa watumishi wa mamlaka hiyo.

“Tuzo hii ina umuhimu sana kwetu, inachangia kuonesha utendaji wetu unakubalika Kimataifa na ina waonesha walipa kodi kwamba kila shilingi inayokusanywa inafika katika mfuko Mkuu wa Serikali,” alisema.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *