Wazalishaji wa simu aina ya sikanu (smartphone) wanajiandaa kuongeza bei kwenye matoleo mapya ya kuanzia 2026, kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni.

Sababu kuu ni ongezeko la gharama za uzalishaji wa kitunza na kichakata data (chipset) kinachoendeshwa na teknolojia ya akili unde (AI), ambapo kampuni kama TSMC ya Taiwan imewaarifu washirika wake wakiwemo Apple inc kuhusu ongezeko la bei la 5–10% kwenye ‘chipu’ zake.

Hatua hii inatarajiwa kuathiri moja kwa moja gharama ya ‘smartphone’ mpya kuanzia 2026, kwani kampuni kama TSMC huzalisha ‘chipu’ zinazotumika katika mifumo mingi ya hali ya juu ikiwemo simu za iPhone, zinazotarajiwa kutangazwa Septemba 2026.

Aidha, baadhi ya wadau wanaamini gharama hizo zinasababishwa na mahitaji ya vipengele vinavyotumia akili unde (AI) katika ‘smartphone,’ hivyo wazalishaji wanalazimika kuandaa vifaa na vichakataji vyenye nguvu zaidi na vinavyotumia nishati kidogo.

Je, nini maoni yako kuhusu mabadiliko hayo mapya yanayotarajiwa kuathiri usafirishaji, uzalishaji na masoko ya simu za sikanu kuanzia 2026?

CHANZO | The Ecominics Times.

Imeandaliwa na Abubakar Yusuf.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *