Wataalam wa afya pamoja na watendaji wa serikali za mitaa na vijiji mkoani Lindi wamehimizwa kuongeza juhudi katika kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia vyoo bora.
Wito huo umekuja baada ya kubainika kuwa, licha ya jitihada zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali, bado kumekuwa na kaya ambazo hazitumii vyoo bora. Hali hiyo imekuwa ikisababisha mlipuko wa magonjwa na kuathiri vibaya jamii husika.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi