
Angalau watu 11 wameuawa kwa kupigwa risasi katika baa moja nchini Afrika Kusini. Wengine kumi na wanne walijeruhiwa wakati watu wenye silaha walipovamia jengo hilo, lililoko katika mji wa Saulsville, magharibi mwa mji mkuu Pretoria, mapema leo Jumamosi asubuhi. Mtoto wa miaka mitatu ni miongoni mwa waathiriwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Angalau watu watatu wenye silaha wasiojulikana waliingia katika hosteli hiyo ambapo kundi la watu walikuwa wakinywa vinywaji na kufyatua risasi ovyo,” amesema msemaji wa polisi Brigedia Athlenda Mathe.
Sababu za kitendo hicho kiovu hazijulikani, na hakuna mtu aliyekamatwa. Hili ni tukio la hivi karibuni katika mfululizo wa ufyatuaji risasi wa watu wengi ambao umetikisa nchi hii, ambayo tayari imekumbwa na uhalifu, katika miaka ya hivi karibuni.
Watu hao wenye silaha wanaripotiwa kuingia katika jengo hilo saa 10:30 alfajiri kwa saa za huko na kufyatua risasi kwa kundi la wanaume waliokuwa wakinywa pombe. Mvulana wa miaka 12 na msichana wa miaka 16 ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo.
“Ninaweza kuthibitisha kwamba jumla ya watu 25 walmejeruhiwa kwa risasi,” Mathe amesema.
Akielezea baa hiyo kama “sehemu ya unywaji pombe haramu,” ameongeza, “Tunakabiliwa na tatizo kubwa na sehemu hizi zinazouza pombe kinyume cha sheria na bila leseni,” ambapo, amesema, mauaji mengi ya watu wengi hutokea.
“Watu wasio na hatia pia wanajikuta wanapoteza maisha katika hali hiyo,” ameiambia televisehni ya serikali SABC.
Afrika Kusini ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani, ikiwa na vifo 45 kwa kila wakazi 100,000, kulingana na takwimu za mwaka 2023-2024 kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu.
Kati ya mwezi Aprili na Septemba, takriban watu 63 waliuawa kila siku, kulingana na data ya polisi.