#HABARI: Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Kihongosi, amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utu na muda na kutotegemea kwamba viongozi wa chama hawatafuatilia kazi wanazofanya.

Kenani amebainisha kuwa baadhi ya watumishi wa Umma wamekuwa wakilalamika kuhusu ushirikiano wa chama katika kufuatilia utekelezaji wa miradi na kusisitiza kuwa kitendo hicho kinaonyesha ukosefu wa utayari wa baadhi ya watumishi kutekeleza majukumu yao ipasavyo na ni ukosefu wa heshima kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Kenani ameeleza kuwa CCM haitaacha kufuatilia utekelezaji wa miradi na huduma kwa wananchi, kwani miradi hiyo ni sehemu ya ilani ya uchaguzi ya chama na kuwataka watumishi kuwa waadilifu na kuhakikisha fedha zinatumiwa kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *