#MICHEZO: @hoseamchopa amezungumza na Dimitar Pandev amesema kwa upande wake amefurahia kipindi chake akiwa Meneja Mkuu wa klabu ya Simba SC na anasema kilikuwa kipindi cha mafanikio kwa kuifanya timu ya Simba iwe timu inayotawala mchezo pamoja ingawa anakiri changamoto ya eneo la mwisho kushindwa kuzitumia vyema nafasi hivyo lazima dirisha dogo wafanyie kazi changamoto hiyo.
Kuhusu kufanya kazi na ushauri wake kwa Suleiman Matola amesema kwa sasa hilo halimuhusu na hawezi kumshauri Suleiman Matola haoni kama ni sahihi kwake ingawa anawatakia Simba kiujumla kila lakheri na mwisho wa msimu mashabiki wa Simba wawe na furaha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.