Ziara hiyo ya Russell imeangazia hitaji kubwa la watoto wa nchi hiyo. Watoto zaodi ya milioni 2.1 walio na umri chini ya miaka mitano wapo kwenye hatari ya kupata utapiamlo. Watu milioni 9.3 sawa na robo tatu ya wananchi wote wa taifa hilo wanaishi kwakuhitaji msaada wa kibinadamu.

“Nilikuwa katika hospitali pekee ya watoto nchini Juba, na nikaona watoto wachanga na watoto wadogo wanaougua utapiamlo na magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika kikamilifu. Inaumiza moyo,” Russell alisema. “Tunajua jinsi ya kuwaokoa watoto hawa, na niliona jitihada za kishujaa za wafanyakazi wa afya katika hospitali na katika jamii. Kwa kuzingatia na uwekezaji endelevu kutoka kwa serikali na jumuiya ya kimataifa, tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi zaidi.”

Takriban watu milioni 1.3 ni wakimbizi na wakimbizi waliorejea nchini mwao baada ya kukimbia vita nchini Sudan, idadi hii ya watu imeongeza shinikizo la shida ya maji, chakula na huduma za matibabu nchini humo.

“Athari za mizozo na mabadiliko ya tabianchi zinatengeneza dhoruba kamili ya mateso kwa watoto wa Sudan Kusini, katika hali ambayo tayari ilikuwa hatari” amesema Russell, ambaye alisafiri hadi Bentiu kuzungumza na jamii zilizolazimisha kuyahama makazi yao kutokana na ghasia na mafuriko.

Wafadhili wa msaada wa kibinadamuwanajitahidi kutoa msaada wakati wowote na popote inapohitajika, #NoMatterWhat..

OCHA/Giles Clarke

Aliyoshuhudia ziarani

“Nilizungumza na mama mmoja ambaye mtoto wake wa kiume wa miaka mitano anaugua utapiamlo mkali. Alikimbia nyumbani kwake na watoto wake wakati kulipotokea mafuriko. Kitu pekee alichookoa ni mkufu ambao alipewa na marehemu baba yake. Mwanawe sasa anavaa mkufu huo kama kumbukumbu ya babu yake na maisha waliyoyaacha.”

Takriban nusu ya wasichana wa Sudan Kusini wanalazimishwa ndoa za utotoni, na asilimia 65 ya wasichana na wanawake wenye umri kati ya miaka 15- 64 wamewahi kupitia aina fulani ya ukatili. Mkuu huyo wa UNICEF alitembelea kituo cha kusaidia wanawake na wasichana.

“Nilizungumza na wasichana na wanawake ambao wamekumbana na ukatili kwa kiwango kikubwa. Wawili kati yao waliniambia walikuwa wamefikiria kujiua kabla ya kufika katika kituo hicho kinachofadhiliwa na UNICEF,”  Russell alisema. “Waliniambia kwamba kuwa na sehemu salama ya kupokea ushauri nasaha na usaidizi wa rika iliwasaidia kama moja ya njia ya kuokoa maisha yao.”

Zaidi ya theluthi moja za maeneo salama yanayofadhiliwa a UNICEF kwa ajili ya wasichana na wanawake yamefungwa kutokana na kukatwa fedha kutokana na uhaba wa ufadhili.

Mkuu huyo wa UNICEF alizungumza pia na wakina mama ambao watoto wao wana utapiamlo mkali.

Watoto wawili kati ya watano wapo kwenye hatari ya kupata utapiamlo mkali nchi nzima na hususan katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko , mzizo na vurugu. Kutokuwepo na usalama kumesababisha asilimia 25 ya kuongezeka kwa hitaji ya misaada ya kibinadamu mwaka huu hali inayoziacha jamii kila misaaada ya haraka inayohitajika.

Sudan Kusini. Chakula kinashukishwa kupitia angani huko Nyueny, Jimbo la Upper Nile.

© WFP/Peter Louis

Elimu

Watoto milioni 2.8 wenye umri wa kwenda shule wanasalia nje ya shule, mojawapo ya viwango vya juu zaidi duniani. Zaidi ya nusu ya shule hazina madarasa salama, walimu waliopata mafunzo, vifaa vya chooni na maji. Wasichana huathirika kupita kiasi, mara nyingi hulazimika kuacha shule kutokana na ndoa za utotoni, ukosefu wa usalama, na kutokuwepo kwa mazingira salama ya kujifunzia.

Kuwekeza katika elimu ni sharti la kimaadili – na msingi thabiti wa amani. Elimu huvunja mzunguko wa umaskini, hupunguza vurugu, na hujenga utulivu wa muda mrefu. Uwekezaji wa umma lazima utangulize elimu sio tu kulinda watoto leo, lakini kuandaa kizazi kijacho kuijenga upya Sudan Kusini ya kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *