#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamadi Mbega, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bw. Abdallah Nandonde, pamoja na wataalaam wengine kwa kusimamia vyema zoezi la ukusanyaji mapato katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, lilipokuwa limevunjwa kupisha zoezi la Uchaguzi Mkuu.

Akizungumza na Madiwani wa Baraza hilo mara baada ya kuapishwa na kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, pamoja na kuchagua wajumbe wa Kamati za Kudumu, Bw. Mbega amesema Mkurugenzi huyo pamoja na timu yake wamefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni sita kati ya shilingi bilioni tisa kama makadirio ya mwaka wa fedha 2025/26 kitu ambacho anapaswa kupongezwa na kupewa ushirikiano.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *