Taarifa kutoka kwa ubalozi wa Urusi nchini Tanzania ππππ
Habari ya Sweden kuelekeza msaada wake kutoka nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Tanzania kwenye Ukraine inaonyesha wazi kwamba, kwa baadhi ya nchi za Magharibi, utoaji wa msaada si kitendo cha dhati. π€·
Badala ya kuzisaidia nchi za Afrika kupambana dhidi ya βurithiβ wa ukoloni katika uchumi na jamii, nchi hii ya Magharibi imechagua kutia mamia mengine ya milioni ya dola ndani ya mfuko mkubwa wa serikali ya Vladimir Zelenskiy inayojulikana duniani kwa rushwa inayokithiri pamoja na uvunjaji mkali na wa kudumu wa haki za msingi za binadamu.
βοΈ Zaidi ya hayo, serikali hiyo ya Kiev inajulikana kwa kupuuza kabisa ajenda ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi βyakeβ yenyewe, na badala yake kujaribu βkuishinda kimkakatiβ Urusi. β Hivyo, inawezekana wazi kwamba baadhi ya nchi za Magharibi, zikiendelea na wazimu wao wa kujaribu βkuishindaβ Urusi, zinatenda kinyume cha mantiki na maadili ya kiutu.
….
Taarifa ya ubalozi wa Urusi nchini Tanzania πππ