#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema kuwa Serikali haina mpango wa kuzima mtandao wa Intaneti nchini, na kwamba hatua hiyo inachukuliwa tu kama kutatokea tishio kubwa la usalama.

Waziri Simbachawene amesema kuwa hadi sasa hali ya usalama nchini Tanzania inaendelea kuwa shwari, hivyo hakuna sababu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuchukua hatua ya kuzima mtandao wa Intaneti kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema taarifa na mijadala ya taharuki inayosambazwa mtandaoni mara nyingi huwafanya baadhi ya watu kuwa na hofu, huku wengine wakizitumia kwa maslahi ya kupandikiza wasiwasi kwa umma, lakini hadi sasa hakuna viashiria vyovyote vinavyodhihirisha uwepo wa tishio la kiusalama.

Amebainisha kuwa uamuzi wowote wa aina hiyo huhusisha taasisi mbalimbali za usalama, lakini kwa mujibu wa tathmini ya sasa, hakuna sababu yoyote ya kuchukua hatua ya kuzima huduma za Intaneti nchini hivyo wananchi waendelee na shughuli zao kwa utulivu.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *