Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imemhakikishia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kufanya tafiti kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ili kukidhi masoko ya nje ya nchi.

Kauli ya taasisi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. Erick Komba alipokuwa akimpa maelezo ya kina Waziri Kakurwa aliyefanya ziara TALIRI kukagua utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kuangalia tija katika inayopatikana katika ufugaji wa kisasa, ufugaji wa kibishara kutokana na utekelezaji huo.

“Ninahitaji mambo matatu kutoka TALIRI ikiwemi kuzielekeza tafiti zenu katika kuongeza thamani ya mazao ya nifugo na hasa katika kuuza zaidi kwenye soko la nje ili mauzo yaongezeke kutoka tani elfu 14 kwa sasa hadi tani elfu 50 ifikapo mwaka 2030” Ameongeza Balozi Dkt. Bashiru.

Sambamba na hilo Waziri Kakurwa ameitaka TALIRI kutafiti kuhusu uhimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na wizara ya maji ili kuboresha eneo la malisho ya mifugo na maji na kutafiti mkakati wa kuendeleza sekta ya ufugaji wa kuku.

Kwa upande wake TALIRI imesema yaliyoelezwa yako ndani ya uwezo wa taasisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *