Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imemtembelea mjasiriamali Idrisa Chisigwa wa Wilaya ya Bahi kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zake za kikodi, kufuatia malalamiko aliyoyawasilisha mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka siku chache zilizopita.

Katika ziara hiyo, maafisa wa TRA wametembelea biashara ya mjasiriamali huyo iliyopo Bahi pamoja na tawi lake lililopo Manyoni, ambapo walijionea shughuli anazozifanya na kufanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala mbalimbali ya kodi yanayohusu biashara zake.

Kupitia majadiliano hayo, TRA imetoa ufafanuzi wa kina uliolenga kuongeza uelewa sahihi kuhusu mfumo wa kodi kwa ujumla pamoja na namna sahihi ya kutimiza wajibu wa kikodi kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Idrisa ameishukuru TRA kwa kumtembelea na kutoa elimu ya kodi, akibainisha kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa vijana wengi wanaojihusisha na shughuli za kibiashara.

Ameeleza kuwa vijana wengi hushindwa kutimiza wajibu wao wa kikodi kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *