Wafanyabiashara wa samaki kwenye Mwalo wa Mswahili – Mwanza wameeleza kuimarika kwa biashara yao baada ya eneo la soko hilo kuboreshwa na kujengewa banda maalumu la kuwakinga na mvua.

Wakizungumza na Azam News, wafanyabiashara hao wamesema maboresho hayo yamekuwa na tija kubwa katika kuimarisha uchumi.

Awali, biashara zao hasa za samaki ziliharibika mara kwa mara kutokana na kunyeshewa na mvua au kupigwa na jua.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *