Kwa kuendelea kwa uingiliaji kati wa kigeni kushadidi mapigano nchini Syria baina ya makundi yanayomuunga mkono mtawala wa nchi hiyo al-Julani na kundi la Qasad, ukosefu wa usalama utulivu nchini humo umechuukua wigo mpana zaidi.
Vyanzo vya Syria vinaripoti kuongezeka kwa mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa Syrian Democratic Forces (Qasad) na vikosi vya usalama vya serikali ya mpito ya Syria katika mji wa kaskazini wa Aleppo. Watu wanne walijeruhiwa kufuatia kuongezeka kwa mapigano kati ya vikosi vya Qasad na vikosi vya usalama vya mkuu wa serikali ya mpito ya Syria, al-Julani.
Vikosi vya usalama wa ndani vya Wakurdi, vinavyojulikana kama “Asayesh”, katika jiji la Aleppo pia vilitangaza kwamba kituo cha ukaguzi katika Uwanja wa “Al-Shayhan” kilikuwa shabaha ya shambulio la silaha.
Shirika la Haki za Binadamu la Syria linaripoti kwamba raia 16, akiwemo mtoto mmoja, walijeruhiwa wakati wa mapigano kati ya vikosi vya serikali na Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria (SDF) katika vitongoji vya Sheikh Maqsoud na Ashrafiya.
Vyanzo vya ndani pia viliripoti kusikia mlipuko mkubwa katika jiji la Al-Bukamal, lililoko mashariki mwa Deir Ezzor, Syria. Kulingana na chombo kimoja cha habari cha Syria, mtu mmoja aliuawa wakati bomu lililotegwa katika pikipiki lilipolipuka katika kitongoji cha Tuwayba cha Al-Bukamal, mashariki mwa Deir Ezzor.

Matukio ya hivi karibuni nchini Syria yanaonyesha kuwa, ukosefu wa usalama nchini humo umeongezeka kutokana na mzozo unaoendelea kati ya wanamgambo wenye mfungamano al-Julani na vikundi vya upinzani, pamoja na uingiliaji kati wa Marekani na utawala wa Kizayuni. Hatua za makkundi yenye mfungamano na al-Julani zieifanya hali ya mambo hasa usalama nchini Syria kuwa mbaya zaidi.
Kwa upande mwingine, jeshi la Marekani pia limepeleka vikosi vyake katika maeneo yenye utajiri wa mafuta na mipaka ya Syria, na hivyo kuzuia serikali ya Damascus kupata udhibiti kamili wa rasilimali za kiuchumi na kijiografia za nchi hiyo. Uungaji mkono kwa Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria pia umesababisha mgawanyiko kati ya Wakurdi na makundi mengine ya Syria na kuzidisha migogoro ya ndani.
Vikosi vya Marekani pia vimeweka mifumo ya kuzuia mawasiliano na kuvuruga mawasiliano kwenye mipaka ya Syria na Iraq, jambo ambalo limesababisha kuibuka mvutano mpya. Utawala wa kizayuni wa Israel pia umepanua uingiliaji kati wake na uwepo wake wa kijeshi nchini Syria baada ya kuanguka kwa serikali ya Rais wa zamani wa Syria Bashar al-Assad.
Utawala wa Kizayuni umelenga mara kwa mara miundombinu ya kijeshi na usalama ya Syria ili kudhoofisha jeshi la nchi hiyo na mhimili wa muqawama. Kwa kuandaa na kuchochea baadhi ya makundi yenye uhusiano na kabila la Druze kusini mwa Syria, Tel Aviv pia imepandikiza chuki za mvutano na utengano katika maeneo hayo.
Baadhi ya chambuzi zinaonyesha kwamba, utawala wa kizayuni wa Israel pia unatafuta korido ya kutwisha kwa ajili ya usalama na ushawishi wa kiuchumi katika eneo hilo, jambo ambalo litapelekea kuigawa Syria na kusambaratika umoja wa kisiasa. Uingiliaji kati wa Marekani na utawala wa Kizayuni haujaidhoofisha tu serikali ya Syria, bali pia umechochea mgawanyiko wa ndani, na hivyo kuandaa mazingira ya mgogoro huo kuchukuua muda mrefu.

Pamoja na uingiliaji kati wa kigeni, vitendo vya Julani pia vimezidisha mgawanyiko wa kijamii na kisiasa nchini Syria, na mchakato huu umefungua njia kwa mhimili wa Kizayuni-Marekani kuwa na ushawishi na na hivyo kuupandikiza migogoro. Kwa sera zake za ukiritimba na utumiaji mabavu al-Julani amefungua njia ya kuanguka kijamii, kuibuka tofauti za kikabila, na kuongezeka kwa ushawishi wa kigeni nchini Syria.
Kwa kuendelea kukandamiza jami za walio wachache, kuwaondoa wasomi wa kisiasa, na kutegemea sana usaidizi wa kigeni, al-Julani amezidisha mgogoro wa kisiasa, kiusalama, na kijamii nchini Syria. Mwaka mmoja baada ya kuanguka kwa uutawala wa Rais Assad, Syria imeporomoshwa kutoka “mchezaji wa kikanda” hadi “uwanja wa ushindani wa kikanda na kimataifa.”
Matukio ya mwaka uliopita yanaonyesha kwamba, kuanguka kwa serikali ya Assad sio tu kwamba, hakukuhitimisha mgogoro wa Syria, bali uingiliaji kati unaoendelea wa mhimili wa Marekani na Uzayuni umeanzisha na kuimarisha awamu mpya ya kutokuwa na utulivu na usalama, kusambaratika wa kijamii, na kushadidi tofauti za kidini nchini humo.