Watanzania wametakiwa kuendelea kuienzi na kuitunza tunu ya amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio msingi wa taifa kupiga hatua kimaendeleo.
Hayo yamesema na Viongozi wa Dini na Serikali wa Mkoa wa Simiyu akiwemo, Shekhe wa Mkoa huo, Issa Kwezi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha na Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa.
Viongozi hao wamesema hayo hivi karibuni Wakiwa ibada iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini, lengo ikiwa ni kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza amani na mshikamano na kumuombe Baba mzazi wa Mbunge huyo, Daudi Kungu Kadogosa ambaye kwa sasa ni Marehemu.