Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mkoani Mbeya, kupitia Kituo cha Uendelezaji wa Teknolojia, limezindua mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu unaolenga kupunguza na hatimaye kuondoa matumizi ya zebaki, kemikali inayotajwa kuwa hatarishi kwa afya za wachimbaji wadogo.

Uzinduzi wa mtambo huo unalenga kulinda afya za wachimbaji wengi wanaojihusisha na uoshaji wa dhahabu kwa kutumia zana duni, hali inayoweka maisha yao katika hatari kubwa kutokana na athari za zebaki kwa binadamu na mazingira.

Mtambo huo, ambao ni wa kwanza kuzinduliwa mkoani Mbeya, umetokana na maboresho ya vifaa na mazingira ya kazi ndani ya karakana ya kituo hicho, ambapo wataalamu wa ndani walibuni na kutengeneza teknolojia hiyo kulingana na mahitaji halisi ya wateja wao ambao ni wachimbaji wa dhahabu.

AzamTVUpdates
✍Kakuru Msimu
Mhariri |@ claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *