Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Nyanda za Juu Kusini imefanikiwa kukamata mifuko zaidi ya 2,000 ya mbolea isiyokidhi viwango, ikiwemo mbolea inayotakiwa kutumika nchini Zambia.

Mbolea hizo zimekutwa kwenye godauni la kuhifadhia mazao na nyingine zikiwa ndani ya gari katika Halmashauri ya Tunduma, wilayani Momba, mkoani Songwe.

Kwa mujibu wa Afisa Udhibiti Bora wa Mbolea kanda ya nyanda za juu kusini, Heneliko Lenatus, ukaguzi ulibaini pia shughuli za ufungashaji upya wa mbolea zisizofaa kwa matumizi ya mazao.

Mbolea zilizokamatwa ni pamoja na NPK mifuko 1,087, D-Compound mifuko 483, DAP mifuko miwili na mifuko 640 iliyokutwa kwenye gari.

✍ Joyce Lyanda
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *