Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mkandarasi wa kampuni ya Bugeta Engineering Ltd kwa tuhuma za kughushi mkataba wa ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo na mabweni katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, iliyopo kata ya Parangu, Halmashauri ya Songea Vijijini.
Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 417 ulitakiwa kukamilika mwezi Oktoba 2025, hata hivyo ukaguzi umebaini kuwa hadi sasa ujenzi umeishia katika hatua ya msingi pekee.
Taarifa hizo zimebainika kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika shule hiyo, ambapo aligundua dosari na kuagiza mkandarasi huyo ashikiliwe na mkataba kuvunjwa.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates