Serikali imewataka wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu katika Ziwa Victoria kujisalimisha na kuacha matumizi ya zana zilizopigwa marufuku kabla ya kuanza kwa operesheni kabambe ya ukamataji.

Akizungumza na wadau wa uvuvi mkoani Mwanza, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Bashiru Ally, amesema operesheni hiyo itawalenga wavuvi wanaotumia makokoro na zana nyingine zisizoruhusiwa kisheria.

Amesema baadhi ya wavuvi wamekiri kuendelea na vitendo hivyo, hali inayohatarisha uendelevu wa rasilimali za uvuvi.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *