Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibingwa za moyo ambapo takribani wagonjwa 1,000 hupatiwa huduma kila siku.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar Group, Dkt. Tulizo Shemu amesema wagonjwa hao hupokea huduma mbalimbali ikiwemo uchunguzi wa umeme wa moyo na upasuaji wa moyo kulingana na mahitaji yao ya kitabibu.
Dkt. Shemu amesema kuanzishwa kwa JKCI kumeongeza upatikanaji wa huduma za moyo na kusaidia wananchi wengi kupata matibabu kwa wakati.
✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates