Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe ameagiza UDART kuhakikisha kuanzia leo usafiri wa Mwendokasi unafika Mbezi hadi Mloganzila, ili kuondoka kero ya usafiri iliyopo kwa sasa na kutengeneza vituo vya muda vya kukatia tiketi.

Prof. Shemdoe ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua fedha iliyotolewa na Serikali zaidi ya shilingi Bilioni 1.2, kwaa jili ya ununuzi wa vipuli vya ukarabati wa mabasi ya Mwendokasi yaliyoharibika..

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa UDART Pius Ng’ingo ameahidi kutekeleza maagizo hayo mara Moja, huku akiwaomba wananchi kutumia vizuri usafiri huo na kuacha tabia ya kuharibu miundombini ya usafiri, huku akiweka wazi kuwa hadi sasa magri 49 yameingia nchini hivyo yatasaidia kuondoa changamoto iliyopo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *