Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo amekutana na Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo la kuweka mikakati ya kuhakikisha msimu mpya wa masomo unaanza kwa ufanisi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee, Mhe.Mpogolo amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema katika kuwapokea wanafunzi, uwepo wa miundombinu thabitii , usimamizi thabiti wa taaluma na nidhamu, pamoja na uwajibikaji wa wakuu wa shule katika kusimamia mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji.

Aidha kwa Upande wake Mkurugenzi wa Halimashauri ya jiji la Dar es Salaam Ndug; Elihuruma Mabelya amesema Serikali imetenga zaidi ya Shilingi bilioni 10 kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya Elimu katika Jiji la dar es salaam

Mkurugenzi Mabelya amesema kiasi cha shilingi bilioni 6.2 kimetengwa kujenga na kuboresha miundombinu upande wa elimu sekondari huku kiasi cha shilingi bilioni 4.5 kikiwa kimetengwa kwa upande wa elimu msingi.

“Ni jukumu letu kuhakikisha tunakwenda kutekeleza wajibu wetu, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameweka fedha nyingi katika Halmshauri hii ili kila kata na kila eneo lipate huduma ya elimu”. Alisema Mabelya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *