Rais wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kutawala vichwa vya habari za kimataifa baada ya kufanya mazungumzo ya simu na Rais wa Colombia, Gustavo Petro, siku chache tu baada ya kutoa kauli kali za vitisho dhidi ya nchi hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika kipindi nyeti, wakati mvutano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Colombia ukiwa bado haujatulia.
Wachambuzi wanaeleza kuwa hatua hiyo inaashiria jitihada za kupunguza mivutano na kurejesha mawasiliano ya kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm