Watumishi wa halmashauri wakiwemo wakurugenzi watendaji na madiwani mkoani Lindi wametakiwa kutumia ipasavyo mafunzo ya uongozi yaliyotolewa kwa madiwani, ili kutatua changamoto za kiuongozi zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya maendeleo.
Imeelezwa kuwa matumizi sahihi ya mafunzo hayo yatasaidia kupunguza migogoro iliyokuwa ikijitokeza baina ya madiwani na baadhi ya watumishi wa umma, na hivyo kuboresha mshikamano, uwajibikaji na ufanisi katika uongozi wa halmashauri.
#AzamTVUpdates
✍Omari Mikoma
Mhariri | @claud_jm