“Taarifa zetu zipo wazi lakini makampuni mengi kama mtakumbuka kipindi cha mwanzo kweli walikuwa hawalipi kodi. Na kuna kodi inalipwa baada ya kampuni kuanza kupata faida.

“Ni kweli makampuni mengi yalikuwa hayalipi kodi yalipokuwa yakianza uzalishaji. Lakini tangu tumeanza kutoa ripoti zetu mwaka 2013 na mwaka 2014 tulitoa ripoti ikaonyesha kweli makampuni yote makubwa hayakuwa hayalipi kodi.

“Baada ya kutoa ripoti tuliishauri serikali na CAG yeye ndiye anayekagua na alikutana na makampuni waliongea na walikubaliana kuanzia mwaka 2014 makampuni yote makubwa yalianza kulipa kodi.

“Sisi hatukusanyi mapato lakini ni kichochezi cha kuisaidia serikali ikusanye mapato yake”- Mariam Mgaya- Katibu Mtendaji Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi Uwajibikaji  katika rasilimali za Madini,Mafuta na Gesi Asilia.

#LiveonClouds360
#LainiYawana
#Clouds26Nyoosha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *