#HABARI: Mama Maria Mtatuu Hango ametoa ushuhuda mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, kuhusu dhuluma anazofanyiwa katika masuala ya mirathi. Akizungumza kwa machungu wakati wa Kliniki ya msaada wa kisheria inayofanyika mkoani Singida, ameeleza namna alivyopoteza haki zake zote.

Mama Maria amebainisha kuwa mgogoro huo umempelekea kufukuzwa hata katika nyumba aliyokuwa akiishi, jambo lililomlazimisha kutafuta msaada wa kisheria ili kupata haki yake.

“Nina kesi ya mirathi, nimedhuluwa kila kitu, na hata nyumba niliyokuwa naishi nikafukuzwa,” alisema Maria kwa uchungu mbele ya Waziri.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *