#Habari: Mshauri wa Wamachinga, Bodaboda, na Mamalishe, Shaban Matwebe, amewasilisha changamoto mbalimbali za makundi hayo katika kongamano lililofanyika. Katika wasilisho hilo kwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, Matwebe alisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja na mifumo ya kusaidia makundi hayo kiuchumi ili kuwavusha kutoka katika hali ngumu waliyonayo sasa.
Matwebe alitoa ombi maalum kwa Waziri Mkuu akitaka SACCOS ya Dar es Salaam itumike kama mfano wa kuigwa na kusambazwa katika mikoa mingine mikubwa nchini. Alitaja mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, na Dodoma kama maeneo muhimu ambayo yanahitaji kuwa na mifumo kama hiyo ya SACCOS ili kuwasaidia wajasiriamali wadogo kupata huduma za kifedha na kujikwamua kimaisha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.