#HABARI: Serikali, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetoa wito kwa vijana na wanafunzi katika shule na vyuo nchini kutoa kipaumbele kujiunga na vyama mbalimbali vya kijamii, hususan Chama cha Skauti Tanzania. Hatua hiyo inatajwa kuwa ni nguzo muhimu katika kutoa malezi bora na kuimarisha maendeleo ya vijana ili waweze kuwa wazalendo wa kweli kwa taifa lao.

Wito huo umetolewa na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania, ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akizungumza mkoani Pwani, katika Mkutano Mkuu wa saba wa chama hicho wa mwaka 2025 uliofanyika wilayani Kibaha.

Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *