Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma imefanikiwa kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa vikundi 30 kati ya 61 vilivyoomba na kukidhi vigezo, ambapo jumla ya shilingi milioni 315 zilitolewa mwaka 2025 kwa lengo la kuinua uchumi wa wananchi.

Takwimu hizo zimetolewa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo, Godfrid Nkuba, ambaye amesema kuwa idadi ya vikundi vilivyonufaika bado ni ndogo ikilinganishwa na vikundi 61 vilivyokidhi vigezo kati ya jumla ya vikundi 128 vilivyosajiliwa katika kipindi hicho.

Nkuba ameongeza kuwa bado kuna haja ya kuongeza juhudi katika utoaji wa mikopo hiyo ili kuwezesha vikundi vingi zaidi kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotolewa na serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *