Mdau wa masuala ya elimu Hussein Mnyagatwa, amewataka wazazi kusimamia kwa karibu matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watoto wao ili kuhakikisha yanachangia maendeleo ya elimu zao.

Mnyagatwa amesema mazingira yanayowazunguka watoto, hususan katika mitandao ya kijamii, yana mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa mwelekeo wao wa kielimu, hivyo ni muhimu wazazi kuhakikisha watoto wanatumia majukwaa yanayowapatia maarifa na ujuzi unaowasaidia kufikia malengo yao.

✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *