Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) limetakiwa kuwaunganisha wakulima na masoko ya kitaifa na kimataifa ya mazao yao sambamba na kutumia mafanikio waliyonayo ikiwemo benki Yao kuweka miongozo ya ushirikiano na wawekezaji.
Hayo yameeelezwa na Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo wakati wa Mkutano Mkuu wa 30 wa TFC huku Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson Ndiege amewataka viongozi wa vyama vya ushirika kusimamia kikamilifu usajili wa wanachama katika mifumo ya kidijitali ili kurahisisha ufikiwaji wa huduma za ushirika katika maeneo mbalimbali nchini.
Imeandaliwa na Tumie Omary
Mhariri @Moseskwindi