Wananchi wa Kijiji cha Lutukira Halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma, wameiomba serikali kutatua mgogoro na kurekebisha mipaka ya ardhi baina yao na muwekezaji ambaye anadaiwa kuvamia eneo lao Zaidi ya ekari 3,200 walilokuwa wakilitumia kwa shughuli za kiuchumi.