Dar es Salaam. Leo ni tarehe ya mwisho wa mwezi wa kwanza wa mwaka Januari. Bado miezi miwili tena kuumaliza Januari. Huo mwezi mwingine utaanza kesho tarehe 11 hadi tarehe 20. Na wa tatu utaanza tarehe 21 na kuisha tarehe 31.

Katika hali ya kawaida ilipaswa tulipwe mishahara mitatu ndani ya mwezi Januari. Mshahara wa kwanza tarehe 10 Januari. Na wa pili tarehe 20 Januari. Wa tatu ni tarehe 31 Januari. Baada ya hapo tulipwe kawaida kila mwezi.

Ndiyo. Mapito tunayopitia mwezi huu siyo poa. Nimeishiwa kila kitu hapa nilipo tangu 28 Desemba, naishi kwa nguvu za macho siku zenyewe hazisogei. Ni kama wale wana wa Israel na msafara wa Mussa kule Jangwani.

Nilijaribu kuzugazuga na AFCON. Lakini yule refarii kutoka Mali, akanirudisha kwenye shida ya mawazo upyaaaaaa. Janauri imekuwa ngumu sana na kibaya zaidi umri wangu umesogea. So… ni ngumu sana mimi kujitafutia chaka. 

Wakati ule wa balehe ningesaka jimama lolote la mjini linifiche. Lakini umri huu mie ndo nasakwa na bintizi kama ‘shuga dadi’ wao.

Nipo kwenye ‘eji’ ya kuhonga gari, viwanja, nyumba, tiketi ya ndege kwenda ‘shopingi’ Dubai, London au New York.

Ni umri wa kulipia matibabu ya mama wa demu wangu huko India. Huu siyo umri wa kuhonga bia na bando wala kulipa nauli ya bodaboda. Ni ‘eji’ ya kumuagizia dem Mazda CX5, na kuezeka paa la nyumba ya mama mkwe wa Kibosho.

Huu ni wakati ambao mabishoo hawana dili kwa madem wa mjini. Hizo ‘siksi paki’ zitalipa ada? Na kulambalamba lips ndo pango la nyumba? Viuno ndo kuwanunua madaftari na nauli kwa watoto wanaporudi ‘bodingi?’ Hii ‘taim’ ufundi peleka VETA.

Ni umri wa kumpeleka ‘waifu’ na watoto ‘vakesheni’ South Africa. Kisha na mimi kuifuata nyumba ndogo iliyopo Geneva. Ikifanya kazi katika NGO’s ya kutetea na kulinda wanyama wa majumbani. Kazi niliyomtafutia mwenyewe.

Bahati mbaya umri wenyewe huu hauendani na maisha hayo. Yaani nimechakaa kiumri sawa sawa na uchakavu wa mifuko yangu. Ndo maana Januari naiona ni mwezi mmoja wenye miezi mitatu ndani yake. Maana nimepigika kinoma.

Januari ya mwaka huu imekuwa ngumu mapema, kutokana na kile kulichoendelea mwishoni mwa mwaka jana. Gen Z wamefanya ‘instolomenti’ upya ya utafutaji kwa udwanzi tu.

Tunasaka ‘Apu’ mpya kwa ‘gugo au apu stoo’ ili kujua tunaendaje. 
Michongo imekata, fereji la pesa lilisombwa na mafuriko ya 2015. Tumebaki kurukia kila mishe na ajenda iliyopita. Pisi zinachoka kwa utoaji mimba, vipodozi feki, njaa njaa, kukesha kama popo na kutumika sana kimwili kama basi za mwendokasi.  

Na mwezi kama huu pisi kali za Kibongo hazina risiti za ‘iefudii’. Utahudumiwa sawasawa na vile unavyokuja wewe. Ukija kihuni na dozi utapewa sawasawa na uhuni wako. Ukiwa mstaarabu utapewa sawasawa na ustaraabu wako.

Lakini nikuonye tu we lofa kutoka uswekeni huko. Pisi za mjini hapa hazipendi ustaarabu wala ‘usmati’ saana wa kichwani. Hakuna mtu mstaarabu anakesha kama mbu wa malaria. Adabu kwa pisi yenye vimelea vya tungi saa 24 ya nini? 

Bro kama ni ‘hedi masta’ sehemu kuwa makini. Utakutana na pisi imeleta mtoto shuleni hapo, jicho limelegea kama tope la saruji. Na kwa ulofa wako ukajua umepata chuma. Tambua hata makahaba  husomesha watoto kwenye shule za gharama. 

Kuna pisi mjini zina kila aina ya bwana, kuna fundi wa kitandani, kuna mlipa kodi, kuna wa kujionesha naye. Kuna wale wa mechi za kirafiki zenye pesa ndefu lakini, tena hizi ndo nyingi.

Mechi za kirafiki ni zile bwana wa rafikie anapiga naye ‘frendi mechi’ bila ‘kuseviana’ namba. Hizi zipo kwa wanaopenda kukaa baa. Na tena hizi mara nyingi zinachezwa kwenye ‘nyutro graundi’. Ndani ya gari tena kwenye parking katika ‘mamozi’. 

Mke wa mtu anapaki gari Mlimani City, anachukua taksi anasepa.  Baada ya saa kadhaa anaibuka tena akishushwa kwenye mkoko na mtu. Anaingia kwa gari lake na kusepa kurudi homu kupigishana kelele na mumewe. Ndo ndoa za sasa hivi zilivyo. 

Utake ndo hivyo usitake pia ndo hivyo. Stori za waume huchepuka kuliko wake zimepitwa na wakati. Kwa sasa kama ambavyo kilio ni 50/50, basi na hili litaingia ndani ya ajenda ili kurahisisha mengi. Kuna shida kubwa sana huko kaa graundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *