Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movies, Gabo Zigamba, amewataka watu kuacha chuki kwa wale waliowatangulia katika maisha au taaluma zao.
Gabo amesema watu waliokuzidi kitaaluma ama uzoefu watumiwe kama sehemu ya kujifunza.
“Usimchukie mtu aliyekutangulia, mfanye mfano kama mchonga barabara, kisha jipange vyema kufanikisha malengo yako, na kama si lazima, basi usifeli hesabu ya mfano,” amesema Gabo.
Gabo aliongeza kusema, anafahamu fika maneno yake yatapokelewa tofauti kwa baadhi ya wasanii wenzake, ila yatakuwa kwa hisia chanya kwa mashabiki wengi ambao wanaona kinachoendelea sababu wanawazunguka.
“Haya maneno yangu ni funzo muhimu la maisha, hususan kwa vijana wanaojitahidi katika nyanja mbalimbali za kazi na sanaa.
“Lakini wapo baadhi ya wasanii wanaweza kuyachukulia tofauti, ila kikubwa mashabiki wetu ni waelewa wapo ambao watanielewa nini namaanisha sababu wao ndio wanatuzunguka kila kona,” amesema Gabo.