Muhula wa masomo wa mwaka 2026 kwa shule za awali, msingi na sekondari umeanza rasmi nchini. Takribani watoto 1,950,783 wanatarajiwa kuanza darasa la kwanza, huku wanafunzi 937,581 wa sekondari wakiripoti katika shule za mikoa na wilaya mbalimbali.
Ufunguzi wa shule umeambatana na mwitikio mkubwa wa wanafunzi, walimu na wazazi, hali inayoonesha dhamira ya pamoja katika kuimarisha na kuendeleza elimu nchini.
✍George Mbara
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
