Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na jinai zilizofanywa na magaidi mamluki katika machafuko na uvurugaji wa amani uliofanywa hivi karibuni hapa nchini.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akizungumzia machafuko na jinai zilizofanywa hivi karibuni hapa nchini na magaidi waliobeba silaha.

Araghchi ameeleza katika barua yake: “mnamo  Alkhamisi na Ijumaa, tulishuhudia vitendo vya machafuko na ugaidi wa mtindo wa DAESH (ISIS) dhidi ya Iran.”

Waziri wa Mambo ya Nje ameongezea kwa kusema: “maandamano ya amani yaliharibiwa na magaidi mamluki”.

Katika sehemu moja ya barua hiyo, Araghchi ameeleza kwamba, kukatwa watu vichwa na kuchomwa moto wakiwa hai pamoja na magaidi kutumia silaha za moto kwa wingi ni mambo yaliyorekodiwa katika matukio ya hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza bayana: “tunataka vitendo vyote vya kigaidi vilivyofanywa na magaidi viliaaniwe”.

Araghchi amekumbusha kwa kusema: “madai ya Marekani ya kuunga mkono haki za binadamu nchini Iran ni ya upotoshaji na ya kuaibisha”.

Barua hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imesisitiza kwa kusema: “tunataka zipingwe aina zote za uingiliaji wa kigeni dhidi ya Iran umoja wa ardhi yake yote pamoja na maslahi yake”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *