#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Denis Ogesa (28) mkazi wa Nairobi nchini Kenya, kwa tuhuma za kuvunja na kuingia katika tawi la benki ya Azania, iliyopo katika mji wa Namanga wilayani Longido.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amesema mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Januari 14, 2026 muda wa saa 6:40 usiku.

SACP Masejo amebainisha kuwa wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kutekeleza tukio hilo la kihalifu katika benki hiyo, alikamatwa akiwa tayari na fedha za Tanzania zenye thamani ya shilingi 91,280,000 na fedha za Kenya zenye thamani ya 288,700.

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linakamilisha uchunguzi kuhusiana watu alioshirikiana nao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *