Wabunge wapatao ishirini wa Bunge la Uingereza wamelitaka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuiondoa Marekani katika fainali za Kombe la Dunia 2026, licha ya kuwa mwenyeji mkuu, kwa sababu ya mienendo ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na ukiukaji wake wa mamlaka ya nchi huru.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, wabunge kutoka vyama kadhaa wamemtaka Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kuiondoa timu ya taifa ya Marekani katika mashindano hayo, wakisema kwamba Washington inapaswa kubeba dhima ya sera zake za kigeni.

Wabunge hao wa Uingereza wamesisitiza kwamba mashirika ya michezo ya kimataifa hayapaswi kutumiwa kuhalalisha au kurekebisha ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Wameonya kwamba sera hizo zinadhoofisha mfumo wa kimataifa unaozingatia sheria, wakiashiria wasiwasi wao kuhusu vitisho vya Marekani dhidi ya mamlaka ya kujitawala ya nchi kadhaa kama Venezuela, Iran, Mexico, na nyinginezo.

Trump na Gianni Infantino

Wabunge hao pia wamelaani vitisho vya siri na vya wazi vinavyotolewa na maafisa wa Marekani dhidi ya mataifa huru.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanasema itakuwa viguvu sana kutekelezwa matakwa ya wabunge wa Uingereza, kutokana na vikwazo vikubwa vya kisiasa na kimfumo vinavyohusiana na Marekani kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico. Hasa ikizingatiwa kuwa, Marekani itakuwa mwenyeji wa mechi 78 kati ya 104 za mashindano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *