#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, faini ya shilingi 500,000 fidia shilingi 2,000,000 na viboko viwili, Mtuhumiwa Ikalala Masololo Shagembe maarufu Mabula mwenye umri wa miaka 20 mjasiriamali na mkazi wa Gezaulole baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba binti mwenye umri wa miaka 16, mwanafunzi wa kidato cha kwanza.
Awali imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo Februari,2025, huko Gezaulole Manispaa ya Kigamboni baada ya kumuomba binti huyo waliyekuwa wanaishi nyumba moja kama familia, kuwa aliingie chumbani kwake kwa lengo la kumkunjia nguo.
Wakati huo wazazi wa binti huyo hawakuwepo nyumbani na mara baada ya kuingia chumbani alifanikiwa kumbaka na kisha kutoweka kusikojulikana.
Binti aliogopa kumweleza mama yake juu ya tukio hilo, hivyo aliondoka na kurudi shule baadae akagunduliwa kuwa ni mjamzito alipohojiwa akaeleza kuwa alibakwa na Mabula.
Mh. Janeth Mtega Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, amesema kuwa Mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa, ambapo umeweza kumtia hatiani Mtuhumiwa huyo kuhusika na kosa la kubaka, na kupelekea kumpa mwanafunzi mimba hivyo ameamuru Mtuhumiwa huyo atumikie kifungo hicho, kulipa faini, fidia na viboko ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.