#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Mboni Mhita amewaelekeza watendaji wa Serikali, watumishi wa Sekta ya Afya na wawakilishi wa wananchi katika sekta mbalimbali, kuanza kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa wote kwa kutoa elimu sahihi ya Bima hiyo kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ameyasema hayo, katika kikao kazi cha kamati mbalimbali za utekelezaji wa afua za afya wakiwemo madaktari, wakuu wa wilaya na wakurugenzi, kamati ya amani ya mkoa na watumishi wa taasisi binafsi wanaojishughulisha na utoaji wa huduma za afya.

Pia amewaelekeza watumishi wa sekta ya afya kuhakikisha huduma zinazotolewa ziwe zinakidhi mahitaji ya wagonjwa na kushirikiana na makundi mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi kuhuisiana na kujiunga na Bima ya Afya kwa wote.

Aidha, amesema Serikali imeandaa mpango maalum wa kugharamia wananchi wa sio na uwezo kupitia mpango wa TASAF ambapo kila Mtanzania anaende kunufaika na Bima ya Afya kwa wote.

Katika muktadha huo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amewaelekeza wakuu wa Wilaya tatu, zinazounda mkoa huo kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri na waheshimiwa madiwani kuhakikisha elimu ya Bima ya Afya kwa wote inafika kwa wananchi na kujiunga na mpango huo kama maelekezo ya Rais Dkt. Samia yalivyoelekeza.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *