#HABARI: Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye pia ni mwanafamilia wa marehemu Mzee Edwin Mtei, amejibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa mitandaoni zikidai kuwa CHADEMA haijapewa nafasi na hadhi inayostahili katika taratibu za kumuenzi muasisi wa chama hicho kabla ya mazishi yake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mbowe amesema anasikitishwa na taarifa hizo akizitaja kuwa ni za uongo na zenye nia ya kuuchafua msiba huo, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu wala kundi lililotengwa katika maandalizi ya mazishi ya marehemu Mzee Mtei.
Mbowe amesema familia inapenda kuona mwili wa marehemu ukipumzishwa kwa amani bila malumbano yoyote, akibainisha kuwa CHADEMA imepewa nafasi kubwa katika taratibu zote kuanzia zoezi la kuuchukua mwili Mochwari hadi shughuli za kumuaga na kumuenzi marehemu.
Mazishi ya Mzee Edwin Mtei yanatarajiwa kufanyika kesho, Jumamosi, katika makaburi ya nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha.
(Feed generated with FetchRSS)